Rais Museveni ampendekeza Jenerali Muhoozi kuwa mrithi wake


Rais Yoweri Museveni wa Uganda aliiambia Kamati Kuu ya chama tawala NRM kuwa, anapendekea mwanawe wa kiume ambaye pia ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa mrithi wake. 

 Hatua hii imezua mjadala miongoni mwa raia na wadau wa siasa nchini Uganda.

Wafuasi wa Jenerali Muhoozi Kainerugaba wameukaribisha msimamo huo wa Rais namna anapoeleza na Godfrey Kabbyanga, kiongozi katika vuguvugu la kisiasa la PLU linaloongozwa na Jenerali Kainerugaba.

“Sisi kama watu wa PLU tulikuwa tunasubiri hilo kabisa. Kwamba tumsikie Mzee anasema nini.” Amesema Godfrey Kabbyanga.

Dkt. Robert Ojambo, mhadhiri wa historia kutoka Chuo Kikuu cha Kyambogo, ana mtazamo tofauti na Bw. Museveni.

“Lazima waache watu waamuwe wenyewe. Hii sio nchi ya ufalme na ufalme umepitwa na muda. ” Amesema Dkt. Robert Ojambo, mhadhiri wa historia kutoka Chuo Kikuu cha Kyambogo

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Akoal Amazima, anatoa maoni yake.

“Ana ushawishi wa kisiasa kwa sababu ana vuguvugu la kisiasa ambalo lina nguvu kubwa sana.” Ameeleza Akoal Amazima, Mchambuzi wa masuala ya kisiasa.

Raia wa Uganda nao wamekuwa na kauli tofauti kuhusiana na suala hili.

“Rais anastahili kuwacha watu wenyewe waamuwe ni nani wanataka awe Rais. Rais amekuwa akimsfia mwanawe sana, nadhani anaona kwamba ni yeye anayestahili kumrithi.” Wamesema baadhi ya raia wa Uganda. 

Hivi karibuni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba alikuwa Mashariki mwa Uganda, ambapo aliomba kuungwa mkono ili awe mgombea wa uraisi mwaka wa 2031 huku wafuasi wake wanakusanya saini milioni 20 ili kuonyesha kiwango cha uungwaji mkono alionao kote nchini.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi