Katibu tawala wa mkoa wa mtwara awataka tehama na maafisa mawasiliano wa serikali kuzingatia miiko na maadili ya taaluma zao.

Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda amewaagiza na Kuwataka Maafisa Tehama na Habari na Kufanya kazi kwa kuzingatia Miiko na Maadili ya Taaluma yanayoelekeza utoaji wa taarifa na matukio ya shughuli na miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao ili kuhabarisha umma kupitia taarifa sahihi.    

Katibu Tawala Luanda,ameeleza hayo wakati akifungua Mafunzo ya Uanzishaji na Uendeshaji wa Tovuti kwa Maafisa Tehama na Maafisa Mawasiliano wa ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mikoa,Halmashauri za Manispaa,Miji na Wilaya kwa taasisi hizo za Mikoa ya Kisini ya Mtwara,Ruvuma na Lindi yatakayofanyika kwa Wiki nzima kuanzia Leo,katika Ukumbi wa Mikutano wa Tiffany Diamond Hotel Mjini Mtwara.  

Luanda,amesema ni vyema Maafisa Habari na Tehama kuzingatia Maadili na Miiko ya Taaluma ya Habari katika masuala ya utoaji wa taarifa zilizo sahihi na zilizochungwa kutoka katika Mamlaka husika na chanzo cha kuaminika kwa lengo la kuwatarifu wananchi kuhusu Shughuli na Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayofanyika pamoja na matukio yoyote yanayofanyika katika Halmashauri zao na kuyatangaza kupitia Tovuti na Mitandao mbalimbali ya Kijamii na Vyombo vya Habari.

Amewaeleza na kuwasihi kujituma na kuwa Wabunifu katika utoaji wa Habari kupitia taarifa na matukio mbalimbali kwa kutumia kikamilifu vitendea kazi vilivyopo,"naomba mjitahidi sana kutoa taarifa kwa nyakati hizi za ukuaji wa Teknolojia hususan matumizi ya simu za Viganjani ama Mkononi ambazo zina uwezo wa kupiga picha nzuri za Mnato na Video zenye ubora na kuzirusha katika mitandao ya jamii"

.Alifafanua na kisisitiza Alfred Luanda.Awali akitoa Maelezo ya Utangulizi kuhusiana na Zoezi zima la Mafunzo ya Tovuti kwa Maafisa Habari na Maafisa Tehama,Kiongozi wa Mafunzo haya kwa Mikoa ya Kanda ya Kusini,Edgar Mdemu ambaye na Afisa Tehama wa Mkoa wa Simiyu alisema Mafunzo ni muhimu sana kwa Maafisa Tehama na Habari ili kuziwezesha Tovuti zote za taasis husika kufanya kazi na kuwa na taarifa za kutosha ikiwemo taarifa na habari mpya za kila siku.

Alifafanua na kueleza kuhusu lengo la Serikali kuimarisha na  kuboresha mifumo ya mawasiliano ya sekta za Umma kupitia ufadhili wa mradi wa Wamarekani USAID Ps3 kwa kwa ushirikiano na Tanzania,kwa uratibu na usimamizi wa Wakala wa Serikali Mtandao na Tamisemi,kwa lengo na madhumuni makubwa ya kuhakikisha kila taasis katika Mamlaka za Serikali za Mitaa inakuwa na Tovuti iliyohai.

Mdemu alieleza pia kwamba Mafunzo haya yanatolewa katika mgawanyo wa Kanda tank ( 5) Mikoa Kanda ya kati ya Dodoma ,Mikoa ya Kanda ya Morogoro,Mbeya na Kanda ya Kigoma,ambapo Mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Simiyu,Mwanza,Mara,Kagera na Shinyanga zimeshafanya Mafunzo haya kwa Maafisa Tehama na Habari na Tovuti za Halmashauri na Mikoa hiyo zimekwishazinduliwa na zinafanyanya kazi kikamilifu.