Dogo Janja anogesha tamasha la urithi wetu


Na Ferdinand Shayo, Arusha
Hitmaker wa Banana, Dogo Janja ametikisa viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha katika Tamasha la Urithi Wetu ambapo Vijana waliokuwepo katika viwanja hivyo walishindwa kujizuia na kumfuata msanii huyo katika Jukwaa kuu.

Idadi kubwa ya vijana waliodhuria tamasha hilo walionekana kupagawa zaidi na Dogo Janja huku wapiga ngoma wenye umri wa makamu wakisogea karibu kushuhudia show ya msanii huyo ambaye alikua kivutio.

Dogo Janja ambaye asili yake ni Arusha amewaambia Wanahabari kuwa amekua akipenda kula vyakula vya asili ya utamaduni ikiwemo viazi, ugali ambavyo vimemfanya awe na nguvu na afya .

Pia amegusia kuwa huwa chakula anachopikiwa na mke wake Irene Uwoya ni ndizi na siku zote amekua akifurahia kula vyakula vya nyumbani vya asili.
Mpya zaidi Nzee zaidi