Afisa Elimu Mkoa kagera bw, Aloyce Kamamba amesema kuwa umoja na mshikamano ni moja ya mbinu walizozitumia kuhakikisha mkoa unapata matokeo mazuri ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka Jana.
"kwanza tulijiwekea malengo sisi kama mkoa, kisha nikazunguka mkoa mzima ninaongea na maafisa elimu wilaya, Tarafa, Kata na kuongea na walimuu wakuu wa shule za misingi na wakuu wa sekondari na walimu wa taaluma kwa siku 29 ili kuwaeleza malengo ambayo tulijiwekea kitaaluma sisi kama mkoa kagera" Alisema kamamba.
Kamamba amesema kuwa walihakikisha kuwa nia ya mkoa inatimia ya kuongeza kiwango cha ufaulu kwa kuwaagiza walimu kufundisha kwa bidii na kutoa mitihani ya majaribio kwa madarasa yenye mitihan kama darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne, na kidato cha sita ambapo walimu walitimiza malengo hayo na kufanikisha wanafunzi kidato cha nne mwaka Jana kufanya vizuri.
Aidha Afisa Kamamba amewataka wanafunzi wa jinsia ya kike kutojihusisha kabisa na masuala ya mapenzi kwa kisingizio cha kutembea umbali mrefu kwenda kufuata elimu hali ambayo inawapelekea kuingia kwenye mahusiano na waendesha pikipiki wakiwadanganya kuwa watakuwa wanawapeka bure shuleni matokeo yake wanapata mimba na kukatishwa masomo na kuanza kuangaika mitaani.