Manchester United yapata pigo

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amethibitisha kuwa Alexis Sanchez atakua nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne au sita kwasababu ya kuumia goti.

Sanchez alilazimika kutolewa kipindi cha pili kwenye mchezo wa Manchester United dhidi ya Southampton ambapo United iliibuka na ushindi wa bao 3-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza uliochezwa Jumamosi.

Akiongea kuelekea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 dhidi ya PSG Jumatano, Solskjaer "amesema Ilikuwa ni ugonjwa mbaya wa magoti, hivyo ni wiki nne au wiki sita. Natumaini atapona haraka."
Mpya zaidi Nzee zaidi