Serikali yatoa zaidi ya bilioni moja kujenga Shule Kigoma


Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kujenga na kukamilisha miundombinu ya Shule za msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua Ujenzi wa vyumba vya madarasa ulioanzishwa kwa nguvu za Wananchi katika shule ya sekondari Janda iliyopo katika kata ya Janda Wilayani Buhigwe.

Waziri Ndalichako amepongeza hatua hiyo ya wananchi nakusema kuwa tayari Wizara kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo(EP4R) imeingiza fedha zaidi ya shilingi milioni Mia Tisa   kwenye akaunti ya Halmashauri ya Buhigwe ambazo zitatumika kuanza ujenzi wa shule mpya msingi yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 945 na kundeleza ujenzi wa miradi mingine ya shule ambayo haijakamilika

“Kwanza niwapongeze wananchi wa buhigwe kwa hatua hii,Hapa  kwenye Halmashauri ya Buhigwe bado kuna kazi kubwa ya kufanya, ukiangalia idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na idadi ya sekondari zilizopo , bado wanafunzi wengi  wanabaki hivyo nawasihi wananchi endeleeni kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule na serikali itaunga mkono juhudi hizo”, alisema Waziri Ndalichako.

Aidha Waziri Ndalichako ameeleza kusikitishwa na ufaulu duni wa wanafunzi wa kike katika mkoa wa kigoma na hasa  shule ya sekondari Janda na kuwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii.


Mpya zaidi Nzee zaidi