Mgomo wa Madereva wa Daladala katika Jiji la Mbeya umemalizika baada ya Uongozi wa Serikali ya Mkoa kukubaliana na pande zote mbili na kuamuru Bajaji zote kutoka barabara kuu na Polisi kuingia barabarani kukamata Bajaji ambazo hazitafuata sheria.
Jana asubuhi machi 18, 2019 watumiaji wa usafiri wa daladala mjini Mbeya walijikuta katika wakati mgumu baada ya daladala hizo kugoma kuendelea na huduma hiyo wakishinikiza bajaji ziondolewe kwa madai ya kuwachukulia abiria.