Aliyewahi kuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa hakuletwa Chadema na mafuriko.
Lazaro kupiti ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa anaamini katika kushiriki kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania kupitia upinzani.
"Sikuletwa CHADEMA na MAFURIKO. Naamini katika kushiriki kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania kupitia upinzani. Tusikate tamaa. Kesho ni nzuri kuliko jana," aliandika Nyalandu.
October 30, 2017, Nyalandu alitangaza kujiuzulu nafasi ya Ubunge wa Singida Kaskazini na kutangaza kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).
