F Tanzania yatoa msaada wa vyakula Zimbabwe, Msumbiji na Malawi | Muungwana BLOG

Tanzania yatoa msaada wa vyakula Zimbabwe, Msumbiji na Malawi


Serikali ya Tanzania imetoa msaada wa tani 24 za dawa, na tani 214 za chakula kwa nchi za Msumbiji, Malawi na Zimbabwe, kufuatia maafa ya kimbunga na mafuriko yaliyozikumba nchi hizo.

Leo Jumanne Machi 19, 2019 Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wamekabidhi msaada huo kwa mabalozi wa nchi hizo nchini, kisha ikaanza kupakiwa katika ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuisafirisha.

Profesa Kabudi amesema misaada hiyo imetolewa na Rais wa Tanzania, John Magufuli baada ya kupata taarifa za kimbunga kisha kuongea na maraisi wa nchi hizo kujua hali halisi.