Loading...

8/11/2019

Rais Magufuli amsaidia huyu mama deni la Milioni 5 baada ya mwili wa mama yake kuzuiwa kuzikwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Rahel Kitwai Roita ambaye alikuwa akiomba asaidiwe gharama za matibabu anazodaiwa kiasi cha Tsh. Milioni 5 anazodaiwa na hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kufuatia deni hilo kulipelekea kuzuiwa kwa mwili wa marehemu mama yake ambaye alifariki katika hospitali hiyo kipinidi cha nyuma.

Baada ya kusikiliza maelezo yake Rais Dkt. Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru aruhusu mama huyo achukue mwili wa mama yake na deni hilo adaiwe yeye. Rais Dkt. Magufuli ametoa rambirambi ya Tsh. laki tano kwa mama huyo.

Ikumbukwe hii leo Rais Magufuli amefika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokwenda kuwatembelea majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea jana Msamvu mkoni Morogoro.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger