Loading...

9/05/2019

Alichosema January Makamba baada ya Rais Magufuli kutangaza msamaha


Mbunge wa Bumbuli na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amemshukuru Rais John Magufuli kwa msamaha aliomtangazia.

Rais Magufuli alitangaza hadharani kuwa amewasamehe January na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM) baada ya sauti zao za kumsema vibaya kuvuja kwenye mitandao ya kijamii.

January alipoulizwa na kuhusu msamaha huo wa Rais Magufuli, alijibu kwa ujumbe mfupi wa maneno katika simu ya mkononi (sms) kuwa, "Namshukuru Rais."

Uteuzi wa mwanasiasa huyo kijana ulitenguliwa na Rais Magufuli Julai 21, mwaka huu, huku nafasi yake ikichukuliwa na George Simbachawene aliyewahi kuwa Waziri wa Tamisemi katika utawala wa Rais Magufuli.

Lakini jana Rais Magufuli alisema hivi karibuni kuna baadhi ya watu walimtukana kupitia mitandao ya kijamii na baada ya kuzisikiliza sauti zao kwa makini, ajiridhisha na kuthibitisha kuwa sauti hizo ni zao kwa asilimia 100.


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger