ACT Zanzibar wamesema hawapo tayari kufanyiwa hujma dhidi ya ofisi zake



Na Thabit Madai, Zanzbar.

Chama cha ACT Wazalendao kimesema hakiko tayari kuvumilia hujuma yeyote iliyoandaliwa dhidi ya viongozi wake au ofisi zake za kufanyia kazi.

Mshauri mkuu wa chama cha hicho Maalaim Seif Sharif Hamad aliyasema hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari  huko ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 .
Alisema kuwa hawatokubali majengo yanayotumika kama ofisi za ACT Wazalendo kusogelewa seuze kuvamiwa na kuchukuliwa na wahuni.

“Tutayalinda kwa njia yoyote majengo hayo ambayo ni mali za watu mbali mbali waliyoyakabidhi kwa chama chetu kuyatumia kama ofisi halali”alisema Maalim Seif.
 .
Aliwataka viongozi na wanachama wa ngazi zote Unguja na Pemba Mjini na Mashamba kuanzia muda huu kuzilinda ofisi zote za chama chao na kutoruhusu kikundi chochote cha wahuni kusogelea achilia mbali kuzivamia na kuzichukua ofisi hizo.

“Uvunjifu wowowte wa amani utakaosababishwa na wahuni hao kujaribu kuyasogelea majengo yetu tuliyokabidhiwa kihalali,uvunjifu huo  gharama   zitabebwa na wahuni hao na wale wanaowatuma na kuwalinda”alisema amshauri huyo wa ACT.

Kauli hiyo ya Maalim Seif imekuja baada ya chama cha waananchi  CUF kisiwani Pemba kujaribu kutaka kuvamia ofisi za ACT-Wazalendo na kuzichukua na kuzifanya ni ofisi za CUF kwa madai ni ofisi zao.

Jana  ulionekana msafara wa magari ukiongozwa na mdhamini wa chama hicho Musa Haji Kombo ukianzia mkoa wa kusini Pemba kwa nia ya kupachua bendera za ACT na kupachika za CUF.

Baada ya ziara ya CUF kisiwani Pemba wanachama  wa chamacha ACT – Wazalendo walionekana kujitokeza kwa wingi kulinda ofisi zao katika maeneo yote ya kisiwa cha Pemba.

Tumevumilia vya kutosha sasa tumnasema basi,kipindi kirefu tulivumilia kutokana na maslahi ya  nchi lakini tumeona wenzetu hawako tayari kuilinda amani, wakimwaga mchuzi tutamwaga mboga”alisema maalim Seif.

Alisema wanandaa fujo zote hizo kwa malengo ya kuwakamata na kuwaweka ndani viongozi na wanachama wa ACT Wazalendo.

Alifahamisha kuwa chama cha wananchi CUF kimefungua kesi ya madai Mahkama kuu ya Zanzibar  kuhusiana na majaengo hayo na huko wametakiwa kuthibitisha umiliki wa majengo hayo iwapo ni chama chao.

“ Shauri hilo bado linaendelea katika ngazi za mahkama  na kujaribu kuwatumia CUF  kusabisha fujo kwa jambo ambalo tayari CUF wenyewe wamelipeleka mahkamani hakukubaliki na sisi hatukubali hilo”alisema maalim Seif.

Mshauri huyo wa ACT alidai  ujio wa katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM kisiwani Zanzibar Dk Bashiru Ali na kujionaea hali mbaya ya chama chao.

“Baada  ya kuona CCM imepoteza mvuto kwa wananchi wa Zanzibar sasa wameamua kutaka kusababisha fujo kwa kumtumia Lipumba “alisema Malim Seif.

Alisema kwamba kutokana na CCM Zanzibar kukataliwa katika mikoa miwili Pemba na kasha kupoteza nguvu zake katika mikoa ya Unguja sasa wameamua kutoa kauli za vitisho ili kuwakata tama vijana.

“Wananchi wa Zanzibar wamewagomea kusini na Kaskazini Mashariki na Mgharibi na sasa wameamua kungan kwa pamoja kudai mabadiliko ya kweli”alisema Maalim Seif.