Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Halmashauri ya Nachingwea yaridhishwa na urejeshwaji mikopo


Na Ahmad Mmow, Nachingwea. 

Urejeshwaji wa mikopo kutoka katika mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika halmashauri ya wilaya ya Nachingwea umetajwa kuwa unaridhisha. 

Hayo yameelezwa leo mjini Nachingwea na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Hassan Rugwa kwenye mkutano wa baraza la madiwani. 

Rugwa alisema licha ya changamoto ndogo ndogo ambazo ameahidi zitatuliwa, lakini kiwango cha marejesho cha wakopeshwaji ni kikubwa. 

Hali iliyosababisha halmashauri hiyo kuwa nimiongoni mwahalmashauri kumi kitaifa ambazo wakopaji wake wanarejesha  kwawakati. 

Alisema licha ya changamoto ndogondogo lakini kasi ya urejeshaji inaashiria kwamba wakopaji wanatambua umuhimu mkubwa wa kurejesha mikopo. 

Mkurugenzi huyo alisema halmashauri hiyo itaendelea kutoa elimu ili kuondoa changamoto zinazojitokeza. 

Huku akizitaja baadhi ya changomoto hizo kuwa ni baadhi ya waombaji kukosa sifa zinazo wafanya wakopeshwe, kasoro katika baadhi ya miradi na shughuli wanazoombea mikopo na wakopaji wengine kudanganya umri. 

'' Baadhi ya vikundi vya vijana, baadhi ya vijana wamevuka umri wa ujana na baadhi ya maandiko siyo sahihi,'' alisema Rugwa. 

Alibainisha kwamba hata baadhi ya vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu vimeonesha ufanisi mkubwa wa urejeshaji mikopo. 

Kwani vikundi hivyo vilikuwa vinachangamoto ya urejeshaji mikopo. 

Alisema halmashauri hiyo inatambua umuhimu wa kukopesha makundi hayo. Kwakuzingatia ukweli huo katika bajeti yake ya 2020/2021 imetenga  shilingi 223,000,000 kutoka kwenye mapoto yake ya ndani kwa ajili ya kukopesha makundi hayo. 

Huku akibainisha kwamba shilingi 216,000,000 kati ya hizo shilingi 23,000,000 tayari zimekopeshwa kwa makundi hayo. 

 '' Hadi mwezi Machi  jumla ya shilingi  326,000,000 zimekopeshwa.    Kati ya fedha hizo shilingi 110,000,000 zimetokana na marejesho,'' Rugwa alibainisha. 

Rugwa alitoa wito kwa madiwani kusaidia kuhamasisha wakopaji kurejesha mikopo kwa wakati. Kwani kurejesha mikopo siyo jambo la hiyari bali lazima. 

 

Post a Comment

0 Comments