Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa, amesema kuwa Wizara yake inafatilia kwa karibu, malalamiko yaliotolewa na wadau wa tasnia ya Habari juu ya Mkurugezi wa Temeke, Lusabilo Mwakabibi kuwaweka chini ya ulinzi wanahabari wa ITV na Island TV
"Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tunafuatilia malalamiko ya wadau ya tasnia ya habari juu ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusabilo Mwakabibi, kuweka chini ya ulinzi wanahabari. Tunaomba wanahabari wawe na subira wakati tunafanyia kazi suala hili." - Waziri Bashungwa
0 Maoni