F Tetesi za Soka Ulaya leo 12/05/2021 | Muungwana BLOG

Tetesi za Soka Ulaya leo 12/05/2021

Manchester United bado wanaendeleza juhudi za kumnasa mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27. (Football Insider)


Arsenal wanajipanga kumsajili mshambuliaji Mfaransa Moussa Dembele. Mchezaji huyo mwenye miaka 24- yuko Atletico Madrid kwa mkopo kutoka Lyon. (Telegraph)


Roma wamejiunga katika kinyang'anyiro cha usajili wa mlinzi wa Brighton Muingereza Ben White, 23, kwa maelekezo ya mkufunzi wao mpya Jose Mourinho. (Sun)


Chelsea wanatarajiwa kumpatia kocha wao Thomas Tuchel mkataba mpya mpya wa miaka mitatu baada ya msimu huu kufikia tamati. (Mail)


Barcelona wameafikiana na Manchester City kumsaini mlinzi wa Uhispania Eric Garcia, 20, kwa uhamisho wa bila malipo. (Goal)


Inter Milan na Lazio wanamnyatia mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 34. (Calciomercato - in Italian)


Jose Mourinho ana matumaini ya kuungana tena na kipa wa Manchester United na Argentina Sergio Romero, 34, atakapochukua rasmi usukani kama mkufunzi wa Roma. (Express)


Manchester United wanakaribia kumsaini kipa wa Aston Villa Muingereza Tom Heaton, 35, kuchukua nafasi ya Romero. (Sun)


AC Milan wanamtaka mlinzi wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier,28. (Calciomercato - in Italian)

 Real Madrid pia wamemefanya mawasiliano na Tottenham juu ay Aurier, ambaye kandarasi yake na Spurs inakamilika mwaka 2022. (Foot Mercato - in French)


Leeds wamewaambia mahasimu wao wa Ligi ya Primia, Liverpool kusahau kuhusu kumsajili mshambuliaji wao Muingereza Patrick Bamford, 27. (Star)


Mchezaji wa nyota wa Southampton Ryan Bertrand, 31, ananyatiwa na Arsenal, AC Milan na Monaco. (Goal)


Southampton na Leeds wanataka kumsajili Ainsley Maitland-Niles, ambaye msimu huu amekuwa kwa mkopo West Brom kutoka Arsenal. Mshezaji huyo aliye na umri wa miaka 23- anacheza kama kiungo au beki wa kulia. (Mail)


Everton watamruhusu winga wao Theo Walcott kuondoka mwishoni mwa msimu . Mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 32, ambae kwa msimu mzima amekuwa Southampton kwa mkopo hatakuwa na mkataba kuanzia mwezi ujao. (Football Insider)


Fulham wanataka meneja wao Scott Parker na mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic kusalia katika klabu hiyo licha ya kushushwa daraja kutoka Ligi ya Primia. (Sun)


Manchester United wako tayari kuwasilisha dau la pauni milioni 15 kumnunua winga wa FC Nordsjaelland na Ghana Kamaldeen Sulemana, 19. Hata hivyo kuna wasi wasi huenda asipewe kibali cha kufanya kazi Uingereza. (Sun)

Chapisha Maoni

0 Maoni