https://monetag.com/?ref_id=TTIb aliyefungwa kimakosa miaka 42 aachiliwa huru Marekani | Muungwana BLOG

aliyefungwa kimakosa miaka 42 aachiliwa huru Marekani

 


Mwanamume mmoja katika jimbo la Missouri nchini Marekani ambaye alifungwa jela kimakosa kwa zaidi ya miaka 42 kwa mashtaka ya mauaji mwaka 1978 ameachiliwa kutoka gerezani.


Kevin Strickland, mwenye umri wa miaka 62, amekana kuhusika tangu alipokamatwa akiwa na umri wa miaka 18. Alihukumiwa mwezi Juni mwaka 1979.


Bw Strickland alisema akiwa nje ya mahakama: "sikufikiria siku hii ingefika."


Kilikuwa ni kifungo cha kimakoskao kirefu zaidi katika historia ya jimbo, lakini chini ya sheria za Missouri huenda asifidiwe.


Kulingana na data kutoka idara ya kuwasajili wale wanaoachiliwa kutoka jela ambayo imesajili kuachaliwa watu tangu mwaka 1989, pia kifungo hicho kinaweza kuwa cha saba kirefu zaidi cha kimakosa nchini Marekaji.


Siku ya Jumanne jaji aliamrisha kuachiliwa mara moja kwa Bw Strickland kutoka jela babada ya siku 15,487 gerezani.


Mawakili kutoka mradi wa Midwest Innocence ambao wamejitahidi kwa miezi kadhaa kusaidia kuachiliwa kwa Bw Strickland, waliiambia BBC kuwa wamefurahishwa na habari hizo.


Jimbo la Missouri huwafidia tu wale wafungwa wanaoachiliwa kupitia ushahidi wa DNA na wala sio kwa njia ya ushahidi wa kuona kwa macho.


Bw Strickland alihukumiwa kifungo cha maisha jela bila ya kuwepo uwezekano wa kuachiliwa kwa miaka 50 baada ya kuhusihswa na kisa cha wizi kwenye nyumba moja katika mji wa Kansas Aprili 25 mwaka 1978.


Usiku huo wavamizi wanne waliwau kwa kuwapiga risasi watu watatu ndani ya nyumba: Sherrie Black, 22, Larry Ingram, 22, na John Walker, 20.


Muathiriwa wa nne Cynthia Douglas, 20 alinusurika na majeraha baada ya kujifanya amekufa.


Kwa pendekezo la mpenzi wa dada yake, polisi walimkamata kijana Strickland na kisha kumshinikiza Bi Douglas kumchagua kutoka kwenye safu.


Bw Strickland aliwaambia polisi alikuwa nyumbani akitazama runinga. Hakuna ushahidi wa kimwili uliowai kumhusisha na uhalifu huo.


Kesi yake ya kwanza mwaka 1979 iliisha bila kutolewa hukumu baada ya jaji mmoja mweusi kati ya majai 12 kutaka aachiliwe.


Kwenye hukumu yake ya pili yenye majaji wote wazungu Bw Strickland alipatikana na hatia ya kuua.


Miaka kadhaa baadaye Bi Douglas aliweza kukana ushahidi wake mwenyewe na kuandika kwa mradi wa Midwest Innocence, "mambo hayakuwa wazi wakati huo, lakini sasa ninajua mengi ni nigependa kumsadia mtu huyu kama nitaweza."


Lakini Bi Doughlas alifariki kabla ya kukana ushahidi wake dhidi ya Bw Strickland lakini mama yake, dada na mtoto wake wote wameiambia mahakama kuwa alimchagua mtu asiye sahihi.


Waendesha mashtaka katika kaunti ya Jackson walianza kuangalia upya hukumu ya Bw Strickland Novemba iliyopita chini ya sheria mpya ya Missouri - wakapeleka mswada wa kutaka aaachiliwe mara moja.

Post a Comment

0 Comments