Loading...

Aug 31, 2019

Fahamu kilimo bora cha zao la Mtama

Mtama ni kundi la mbegu ndogo aina ya mazao ya nafaka au nafaka ambayo kwa jina la kisayansi unajulikana kama (Sorghum bicolor), ni mazao yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na lishe Mtama hutoa mazao mengi hata kwenye hali ambayo haifai kwa kilimo cha aina nyingine za mazao ya nafaka. Mtama una uwezo mkubwa wa kustahimili ukame.

Mtama unaweza kutumika kwa kuchemshwa na kuliwa kama ulivyo, kusagwa na kutumika kwa uji, kutengenezea vinywaji kama vile bia, kuoka mikate, na aina nyinginezo za vitafunwa. Mmea wa mtama pia hutumika kwa ajili ya malisho ya mifugo kama vile hay  na sileji. Mtama unastawis vizuri kwenye mazingira yenye wastani wa milimita 400 – 700 za mvua kwa mwaka. Pia mtama unavumilia sehemu zinazotuhamisha maji, na unaweza kulimwa sehemu zenye mvua nyingi.

Mtaama unafaa pia kwa sehemu kame zenye wastani wa joto la chini kiasi cha nyuzi joto 18°C, ili kuweza kuota vizuri, na kiasi cha nyuzi joto 25-30°C ili kukua vizuri. Mtama hauwezi kuvumilia barafu. Mtama unaweza kukua kwenye aina zote za udongo. Kwa kiasi kikubwa unafaa zaidi kwenye udongo wa mfinyanzi, lakini pia kwenye udongo ambao una kiasi kidogo cha mchanganyiko wa kichanga. Mtama unaweza kuvumilia uchachu kwenye udongo kuanzia pH 5.0-8.5, na inavumilia udongo wenye chumvi kuliko yalivyo mahindi.

Aina za mtama
Kwa jumla kuna aina zaidi ya 30 za mtama zinazolimwa kama chakula. Mtama hustawi vizuri kwenye joto ikivumilia pia ukame. Hivyo ni nafaka muhimi kwenye maeneo yabisi za Afrika. Katika miaka ya nyuma kilimo chake kiliachwa mara nyingi kwa ajili ya mahindi kwa sababu mahindi huleta mazao makubwa zaidi kwa ekari. Lakini wakati wa ukame mahindi ni hasara na watu hurudi-rudi kwenye kilimo cha mtama.

Aina za mtama zinatofautiana kulingana na rangi zake, kuna nyeupe, nyekundu, na kahawia. Mbegu za asili huwa zinachavushwa kwa urahisi zaidi lakini mavuno yake huwa ni hafifu ukilinganisha na mbegu za kisasa. Hata hivyo, aina za kisasa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi zinapopandwa kwa kufuata kanuni za kilimo bora.

Serena:  Ina punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha kilo 3,000 kwa hekari moja. Ambapo zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.

Seredo:  Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha kilo 5000 kwa hekari moja. Ina uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya kahawia kwenye majani.

Gadam: Inafanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.

Hakika na Wahi:  Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba yalioathiriwa na viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili zinafaa sana kwa kupika ugali.

Utayarishaji wa shamba na kupanda
Kwa kawaida mtama hupandwa kwa kutumia mbegu. Mbegu hupandwa shambani moja kwa moja baada ya shamba kuandaliwa, lakini pia zinaweza kurushwa shambani, kasha zikavurugwa pamoja na udongo. Unapaswa kutayarisha shamba la kupanda mtama, iwe ni kwa ajili ya malisho au chakula kabla mvua za msimu hazijaanza. Zao hili hufanya vizuri zaidi kwenye udongo ulio laini. Linaweza pia kupandwa kwenye udongo ambao haukulimwa vizuri na bado ukaota vizuri.

Nafasi:  Mtama unaopandwa kwa ajili ya malisho, unaweza kupandwa kwa nafasi ya sentimita 75×10. Aina za mtama ambazo zinalengwa kwa ajili ya lishe kwa binadamu na wanyama, zinahitaji nafasi kiasi cha sentimita 60×20. Nafasi hutoa mwanya wa kuwa na kiwango kikubwa cha malisho. Mkulima anaweza kupanda mbegu za mtama kiasi cha kilo 2.4-3.3 kwa hekari moja. Ni mara chache sana mbegu hupandwa kwenye vitalu na kuhamishiwa shambani baadaye.

Kupanda:  Mtama hupandwa mvua zinapoanza kunyesha. Mbegu ni lazima zifukiwe ardhini usawa wa sentimita 3 kwenda chini, hii itasaidia kuepuka kuota wakati ambao si msimu kamili wa mvua. Pia zinaweza kufukiwa kiasi cha sentimita 2 wakati ardhi inapokuwa na unyevu. Mtama unahitaji rutuba ya hali ya juu wakati wa kupanda na wakati wa kuota. Ni vizuri kutumia samadi au mboji iliyooza vizuri wakati wa kuandaa shamba.

Mseto:  Unaweza kupanda mtama mseto na mazao jamii ya mikunde, na kuongeza mboji shambani mwako. Hii inaweza kuwa njia nzuri zaidi ya kupata virutubisho vinavyohitajika. Mseto wa mazao jamii ya mikunde inashauriwa iwe ni kama vile maharagwe, kunde, n.k

Uangalizi na utunzaji
Ni lazima kung’oa baadhi ya mimea inapokuwa na urefu wa sentimita 30, au siku 30 baada ya kupanda, ili kuwa na uhakika wa nafasi ya sentimita 10 kati ya mstari na mstari kwa mtama unaokusudiwa kwa ajili ya malisho, na nafasi ya sentimita 20 kati ya mstari kwa mtama uliokusudiwa kwa ajili ya chakula na lishe ya mifugo.

Palizi ya mkono ifanyike walau mara mbili. Shamba la mtama ni lazima liwekwe katika hali ya usafi na kutokuruhusu magugu wakati wote hasa katika kipindi cha mwanzoni.
Share:

Njia saba za kuwa mfanyabiashara mkubwa


Je unataka kuwa kama MO ??  Fuata hatua hizi 7 utafika alipo MO..

1. Chagua wazo bora la kibiashara.
Wazo bora la kibiashara ndilo litakalo kufanya kuwa mfanyabiashara wa mkubwa. Mara nyingi nimekuwa nikikutana na watu wakisema wanataka kuwa wafanyabiashara na kuishia kusema tu. Ila ukweli ni kwamba katika kuchagua wazo bora la kibiashara ni lazima ujiulize je unataka kuwa mzalishaji wa bidhaa au huduma? Je unataka kuwa mnunuzi na muuzaji?au  je unataka kuwa msambazaji tu ? Hayo yanaweza kuwa miongoni mwa maswali ya msingi ya kujiuliza.

2. Fanya uchunguzi juu ya washindani wako.
Hapa ndipo jicho la tatu linaposhindwa kufanya kazi mara nyingi. Tumekuwa si wachunguzaji wazuri juu ya washindani wetu ila tumekuwa wasikilizaji tu kwa watu wengine juu ya washindani wetu. Ila ikumbukwe ya kwamba fanya uchunguzi wa kutosha ili kujua washindani wako wanatumia mbinu zipi kukuza biashara zao. Hii itakusadia pia kujua ni wapi wanapokosea ili uweze kulizipa pengo hilo. Kwa kufanya hivi kutakufanya ndoto zako za kuwa mfanyabiashara wa kimataifa zitimie.

3. Tafuta mtu wa kukuongoza. (Helpful mental).
Tafuta mtu sahihi wa kukuongoza  na si mtu wa kukukwamisha. Watu wengi tunashindwa kuwa wafanyabishara wakubwa hii ni kutokana tunatafu watu ambao sio sahihi katika kutushauri. Stuka mapema juu ya jambo hili. Na anza kukaa na watu ambao tayari wamefanikiwa kwenye biashara zao watakusaidia sana kufika kule unakotaka kufika kibiashara. Siku zote ukitaka kuruka kama tai, ni lazima ujifunze kama tai wanavyoruka. Kwa maana huyo ukitaka kuwa mfanyabiashara mkubwa kubali kuchukua mwongozo wa wafanyabiashara waliofanikiwa.

4. Tambua biashara inayokua.
 Ukilijua hili ni jambo jema zaidi. Moja ya tatizo kubwa ni kwamba tumekuwa tukishuhudia biashara hazikuwi miaka nenda miaka rudi. Hii ni sababu kubwa ambayo inachangia tusiweze kujua ni kwa jinsi gani tusiwe wafanyabiashara wakubwa. Natamani kuona malengo yako yanabadilishwa kila wakati. Kwa mfano leo unauza nguo kwa kutembeza, ili kuona biashara inakuwa tunataka kuona unapata chumba kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo napo kweli tunasema biashara inakua. Kama unafanya biashara mkoa wako mzima tunatamani kuona unaongeza mkoa mwingine na mwingine katika kusambaza huduma au bidhaa.

5. Panga malengo na mipango ya biashara yako.
Hapa inahusiana na juu ya kuuza, kununua bidhaa au huduma. Lazima malengo ya biashara yako uyapange kila robo ya mwaka ili kugundua kama biashara yako inakuwa au haikui. Na lazima pia katika kupanga malengo yako, utambue baada ya muda fulani biashara yako itakuwa imefika wapi. Kwa mfano ni muhimu kujua biashara yako itakapokuwa baada ya miaka miwili au mitatu mbeleni.

6. Tangaza biashara yako.
Wateja wako ni lazima wajue bidhaa na huduma ambayo unazalisha. Si kujua tu, lengo jingine la kutangaza bidhaa au huduma inamfanya mtumiaji aweze kujua jinsi ya kutumia kitu hicho. Kwa kutangaza biashara wateja huongezeka kwa asilimia kubwa sana na kufanya huduma au bidhaa yako kuweza kupendwa na wengi pia. Matangazo ni njia mojawapo bora ya kukufanya kuwa mfanyabiashara wa kimataifa ikiwa utaitumia vizuri.

7. Jenga mahusiano mazuri na wateja wako.
Jitahidi kulizingatia hili ya kwamba Kauli katika biashara ni mali kuliko hata  pesa. Jali wateja wako na kuwafanya wajihisi kama wanapata bidhaa bure. Kwa kadri utakavyozidi kujenga mahusiano bora na wateja hiyo itapelekea wao kupenda bidhaa zako na hiyo itakusaidia kukuza wateja wengi siku hadi siku.

Ni matumaini yangu umenielewa vizuri hizo ni baadhi ya siri chache kati nyingi zitakazokufanya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Asante sana na usisite kumshirikisha mwingine.
Share:

Jinsi ya kuepuka kunuka mdomo


Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla. Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni uondoa haiba ya kupendwa kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea moja kwa moja na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni mwako.

Chakula unachokula kina athiri hewa inayotoka mdomoni au sehemu nyingine za mwili wako. Baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni. Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba atakuambukiza.

Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya. Asilimia 85 - 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).

Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya protein. Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).

KINACHO SABABISHA HARUFU MBAYA MDOMONI
Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni. (Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula). Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa upumuaji na kisukari. Kinywa kuwa kikavu kutokana na madawa (medications) Kuvuta sigara, kunywa kahawa, ulaji wa vyakula vyenye viungo vikali kama vile vitunguu maji au thaumu.

NAMNA YA KUJUA KAMA UNA HARUFU MBAYA MDOMONI
Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).

Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine. Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini.

Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa. Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.

NAMNA YA KUJILINDA NA HARUFU MBAYA MDOMONI (TIBA) 
Kula vyakula vyenye afya na vyakula ambavyo wakati unakula vinaweza kusafisha kinywa vizuri. Kusafisha meno mara kwa mara au kwa uchache mara mbili kwa siku asubuhi na baada ya mlo wa usiku, hii usaidia kuondoa au kujikinga na harufu mbaya mdomoni.

Vilevile unashauriwa kutumia KISAFISHA ULIMI (tongue cleaner) kusafishia ulimi wako. Tumia bazooka (chewing gum) ambazo husaidia kuongeza kiasi cha mate kwenye kimywa kilichokauka.

Baadhi ya gums zina viungo vinavyoondoa harufu mbaya mdomoni na zingine husafisha kinywa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya. Tumia dawa ya kusukutua mdomoni (mouthwash) kabla ya kulala usiku. Kuwa makini na afya ya kichwa chako kama vile kupiga mswaki vizuri, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno na kumuona daktari kila unapoona una Matatizo ya meno au kinywa au kila baada ya miezi sita kwa uchache.

Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau glass mbili za maji.
Mwone daktari wako ukiona una tatizo la harufu mbaya mdomoni.

NAMNA YA KUJIKINGA NA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI!
Watu wengi husumbuliwa na tatizo la kunuka mdomo bila hata kujijua hivyo kuwa kero kwa wenzao na wakati mwingine hujishushia hadhi mbele ya jamii. Mara nyingi ugonjwa wa kunuka mdomo (Halitosis) husababishwa na uchafu wa kinywa na ulaji wa vyakula usiosahihi lakini ni tatizo linalotibika.

Ni rahisi kulizuia na kuliondoa tatizo la kunuka mdomo iwapo utaamua kufuata kanuni za usafi wa kinywa na unywaji wa maji kwa kufuata kwa makini muongozo ufuatao:

KUPIGA MSWAKI
Kitu cha kwanza kufanya ni kupiga mswaki kwa ukamilifu kila uamkapo asubuhi. Wakati wa kupiga mswaki, utatakiwa siyo tu kusugua meno, bali pia ulimi, sehemu ya katikati hadi karibu na koromeo kwa kusugua vizuri.

Vile vile kila uamkapo baada ya kulala mchana au jioni, hakikisha unapiga mswaki, kwani bakteria wa kinywani, hutawala kinywa kila ulalapo. Mara baada ya kupiga mswaki na kusugua ulimi sawaswa, hakikisha unasukutua vizuri kwa maji, kwani hapa ndipo baadhi ya watu hukosea kwa kupiga mswaki bila kusukutua kwa maji.

KUNYWA MAJI MENGI
Maji ni muhimu sana karibu kila eneo la mwili wa binadamu. Unywaji wa maji ya kutosha kila siku utakusaidia kudhibiti na hatimaye kuondoa tatizo la kunuka mdomo. Unywaji wa maji mengi ni muhimu, hasa kwa wale watu wenye ugonjwa wa kukauka midomo (xerostomia).

Mara nyingi harufu itokayo mdomoni, hutokea tumboni na siyo kinywaji peke yake kama unavyoweza kudhani. Hivyo, kama tumbo litakuwa chafu, hata kama utasafisha kinywa vizuri bado harufu mbaya inaweza kuendelea kutoka. Harufu mbaya ya tumboni hutokea pale tumbo linapokuwa chafu kutokana na kutopata choo kwa muda mrefu. Miongoni mwa mambo yanayochangia kukosekana kwa choo kwa muda mrefu ni pamoja na tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kwa siku, hivyo hakikisha unakunywa maji, kiasi kisichopungua lita moja na nusu hadi mbili au zaidi, kutegemeana na kazi unazozifanya.

Ukiwa na tatizo la kukaukiwa maji mwilini kila mara, mwili hujaribu kutumia njia zake za kiasili kupunguza uzalishaji wa mate ili kuhifadhi maji kwa ajiili ya matumizi mengine, kitendo hicho huchangia kunukisha mdomo kwa sababu ndani ya mate huwa kuna kinga muhimu dhidi ya baktetria wanaonukisha kinywa.

Kwa upande mwingine, ili kuzuia kinywa kunuka pale mdomo unapokuwa umekaukiwa na mate, ni vizuri kutafuna vitu kama bazooka (chewing gum) yoyote ili kuzalisha mate ambayo huhitajika katika kudhibiti bakteria.

MWISHO: Hakikisha unasukutua sawaswa baada ya kula chakula chochote, hata kama ni juisi isipokuwa unapokunywa maji tu ya kawaida. Bila shaka, ukizingatia haya, tatizo ulilonalo la kunuka mdomo litataoweka na kubaki historia.
Share:

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje "Kaduma" afariki dunia


Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani katika serikali ya awamu ya kwanza, Ibrahim Kaduma, 82, amefariki dunia nchini India usiku wa kuamkia leo, Jumamosi.

Waziri huyo wa zamani amedaiwa kuwa alienda India wiki iliyopita kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake kabla ya umauti kumfika.

Enzi wa uhai wake, Kaduma alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri aliwahi kuhudumu katika serikali kama katibu mkuu katika wizara mbalimbali ikiwemo nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje kuanzia mwaka 1975 hadi 1976.

Mchumi na mwanasiasa huyo  alizaliwa mwaka 1937 huko Mtwango, mkoani Njombe na alifamikiwa kupata elimu yake ya juu katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda na University of York kilichopo Uingereza. Marehemu ameacha mjane, watoto watano na wajukuu tisa.
Tukiwa kama Muungwana Blog tunatoa pole kwa familia ya marehemu na Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi....Amiina.
Share:

Ujumbe wa kwanza wa Sugu baada ya kufunga ndoa na mkewe Happiness, "Sasa ni rasmi"Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, ameandika ujumbe wake wa kwanza kwenye mtandao wa Instagram tangu alipofunga ndoa leo (Jumamosi) mchana.

Kupitia mtandao huo Sugu ameweeka picha hiyo hapo juu na kuandika, "Mr & Mrs Joseph Mbilinyi... Sasa ni RASMI zaidi ❤️❤️... #JONGWE#MVMP."

Ndoa ya Sugu na mkewe Happiness Msonga imefanyika katika kanisa la Katoliki Ruanda.

Share:

Matokeo ya mechi zote ligi kuu Uingereza leo, Man City yatembeza kipigo cha "Mbwa Koko"


Klabu ya soka ya Manchester City imetembeza kipigo cha "Mbwa koko" katika ligi kuu ya Uingereza Jumamosi hii.

Timu hiyo ambayo ilikuwa inacheza na Brighton, imeibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Mabao ya City yamefungwa na Kevin De Bruyne dakika ta pili ya mchezo, Sergio Agüero aliyefunga mawili (dakika ya 42 na 55) na Bernardo Silva (79).

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo. 

Southampton (1-1) vs Manchester United
Crystal Palece (1-0) vs Aston Villa
Newcastle United (1-1) vs Watford
West Ham United (2-0) vs Norwich
Chelsea (2-2) vs Sheffield United
Burnley () vs Liverpool
Share:

Chelsea ya Lampard ngoma nzito ligi kuu, washindwa kutamba kwa madogo


Klabu ya soka ya Chelsea imeshindwa kufurukuta katika uwanja wake wa nyumbani Stamford Bridge baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Sheffield United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

Chelsea ndio walikuwa wakwanza kupata mabao yao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Tammy Abraham (dakika ya 19 na 43).

Sheffied United walizawazisha kupitia kwa Callum Robinson aliyefunga dakika ya 46 na Kurt Zouma ambaye alijifunga dakika ya 89 ya mchezo huo.

Huu ni mchezo wa pili kwa Chelsea kutoka sare msimu huu huku akiwa tayari amepoteza mchezo mmoja na kushinda mmoja.
Share:

Akaunti ya Twitter ya muanzilishi wa Twitter yadukuliwa, Chuckling Squad wahusishwa


Wadukuzi kila kukicha wamekuwa wakiwatesa watum8iaji wamitandao ya kijamii sio bongo tu tena hasa watu maarufu zaidi.

Mwanzilishi na mkurugenzi wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Jack Dorsey amedukuliwa akaunti yake ya mtandao huo.

Hata hivyo Kundi la wadukuzi linalojiita Chuckling Squad limedai kuhusika na udukuzi wa akaunti hiyo ya Jack Dorsey. Akaunti hiyo yenye watu zaidi ya milioni nne, ilianza kutumiwa kwa kusambaza taarifa za chuki na kibaguzi kwa kutumia lugha chafu kwa karibu dakika kumi na tano.

Twitter inasema mitambo yake haikufikiwa na wadukuzi na badala yake kulaumu kampuni ya mawasiliano ambayo haikuitaja jina lake kwa kusababisha hitilafu hiyo.

“Nambari ya simu inayohusishwa na akaunti hiyo ilitumiwa kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyosababishwa na kampuni hiyo ya mawasiliano,” imesema taarifa iliyotolewa na Twitter.

“Hali hiyo ilitoa fursa kwa watu wasio na idhini ya kutumia nambari hiyo kuanza kutuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter.”

Chanzo cha habari kutoka Kampuni hiyo ilithibitishia BBC kuwa wadukuzi walitumia mfumo unaojulikana kama “simswapping” kuchukua udhibiti wa akaunti ya Twitter ya Bw. Dorsey.

Huu ni mfumo ambao inatumiwa kuhamisha nambari halisi ya simu ya Dorsey katika laini nyingine- na kuanza kuitumia.

Wadukuzi mara nyingine hutoa hongo kwa wahudumu wa kampuni za mawasiliano au kuwapotosha kupata namabari halisi.

Kwa kuchukua udhibiti wa nambari hiyo wadukuzi waliweza kuandika ujumbe moja kwa moja katika akaunti ya Twitter ya Bw. Dorsey.

Japo siku hisi watumiaji wengi wa mtandao huo wanatumia programu tumishi kwenye simu zao kutuma ujumbe, awali Twitter ilibuniwa katika mfumo wa kutuma ujumbe mfupi- hali inayoisaidia kudhibiti idadi ya maneno mtumiaji anastahili kuandika.

Wadukuzi waliandika nini?

Ujumbe wa chuki na wa kibaguzi – ulitumwa moja kwa moja kwa kutumia akaunti ya @jack, na wengine waka sabaza ujumbe huokwa kutumia akaunti zingine.

Ujumbe mmoja uliashiria kuna bomu limetegwa katika makao makuu ya kampuni hiyo.

Chuckling Squad imewahi kuhusika kudukua Twitter ya mmiliki wa Blog maarufu ya masuala ya urembo James Charles na watu wengine.
Share:

Goodluck Gozbert awajibu wanaodai ngoma yake "Nibadilishe" sio gospel


Muimbaji wa muziki wa injili nchini Goodluck Gozbert amefungukza kuwa hakuandika wimbo wa "Nibadilishe" kwa ajili ya watu waliookoka.

Kiongea kwenye kipindi cha Bongo Fleva cha Clouds FM, Gozbert amesema, “Sikuandika Nibadilidshe kwa ajili ya watu waliookoka.”  

“Wakati naandika Nibadilishe sikufanya kwa ajili ya watu ambao wapo tayari kwenda mbinguni, bali nilifanya kwa ajili ya watu ambao wanajua kila kitu kuhusu dini yake na wanajua kuhusu Mungu na kuna vitu wanashindwa kuvifanya vya kiimani na hawajui kwanini vinawashinda,” ameongeza.


Msanii huyo amesema hayo baada ya watu wengi wamekuwa wakizungumza kuwa wimbo huo haujakaa ki-gospel.
Share:

TAKUKURU yaokoa bilioni 86 tangu mwaka 2015


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa nchini (Takukuru) imeokoa kiasi cha shilingi bilioni 86 zilizotokana na ukwepaji kodi na makosa mbalimbali ya ufisadi tangu mwaka 2015.

Hayo yameelezwa Jumamosi hii na msemaji wa msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika mjini Dodoma.

Dk Abbas amesema kati ya fedha hizo,  Shilingi bilioni 14.6 zimerudishwa serikalini kwa kuwa zimepatikana katika uhalifu na shilingi bilioni 10 zimerudishwa tena serikalini baada ya kuuza magari, nyumba na vituo vya mafuta.

“Takukuru pia wamerejesha zaidi ya Shilingi bilioni 25 zikiwemo fedha zilizopatikana kwa rushwa baada ya washtakiwa kukutwa na hatia, fedha hizo zinarudi kwa Watanzania,” amesema Dk Abbas.

Pia ameongeza kuwa Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA)  imeokoa kiasi cha shilingi bilioni 46.8 zilizotokana na mikataba mibovu waliyoibaini wakati wa ukaguzi.
Share:

Faiza Ally ajibu mapigo baada ya mzazi mwenzake Sugu kuoa, "Hope you will treat me well tonight"


kuna msemo unasema, "Ukisema cha nini basi mwenzako anajiuliza atakipata lini" hilo limejidhihirisha Jumamosi hii baada ya mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi "Sugu" kufunga ndoa na mpenzi wake Happiness Msonga.

Wawili hao wamefunga ndoa hiyo katika kanisa la Katoliki Ruanda Parokia ya Roho Mtakatifu.

Hata hivyo muda mfupi baada ya ndoa hiyo kupita mzazi mwenzake na Sugu, Faiza Ally ameandika ujumbe kupitia mtandao wa Instagram ambao baadhi ya mashabiki wa ubuyu wa mitandaoni wamechukulia ni kama amejibu mapigo.

Kupitia mtandao huo, Faiza ameandika, "Hello beautiful ☺️☺️ Hope you will treat me well tonight 😉👄🥂."
Share:

Mwanamitindo Bongo Ben Breaker atajwa kuwania tuzo nyingine Ghana


Mwaka 2019 huenda ukawa ni waneema kubwa kwa mwanamitindo wa kiume hapa Bongo, Ben Breaker - Baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo za Star QT za Afrika Kusini, amefanikiwa kupata dili jingine nchini Ghana.

Breaker amechaguliwa kuwania tuzo kubwa za nchini humo zinazofahamika kama "Odartey Style and Fashion Awards".

Katika tuzo hizo Ben amechaguliwa kuwania katika vipengele viwili ambavyo ni ambavyo ni Best Icon na People's Choice.

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika mjini Accra, February ya mwaka 2020.Share:

Mrajisi awafunda viongozi wa bodi ya Kahawa


Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Kagera, Robert Makene Kitambo ameutaka uongozi wa bodi ya chama cha ushirika wilayani Ngara kushirikiana na wakulima wa zao la Kahawa kutatua changamoto zinazo wakabili katika zao hilo na kuhakikisha wanalizalisha kwa tija.

Mrajisi huyo amesema hayo leo katika kikao cha kuchagua bodi mpya ya kuongoza chama hicho kufuatia ile iliyokuwepo kumaliza muda wake. Pia ameongeza kuwa ni vema wajumbe wa bodi hiyo kujua kuwa wakulima ndiyo waajiri wao hivyo ni vema kuwatumikia na sio kwenda kuwa juu yao na kusahau majukumu yao yaliyowapeleka hapo.


"Changamoto zilizopo kwenye ununuzi na uuzaji wa zao la kahawa tunazitambua na nimeiagiza bodi ya chama cha Ngara Famers kwenda kuzitatua kero zenu na kuhakikisha mnauza mazo yenu kama serikali inavyoelekeza na kulipwa kwa wakati," amesema Roberty Makene.

Aidha Mrajisi huyo ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inaongea na taasisi za kifedha ili kupeleka huduma za kifedha karibu na mkulima ili kuondoa adha ya kufata mbali malipo yake pale anapokuwa amemaliza kuuza huku akiwaomba wakulima kufungua akaunti za benki ambazo hazina makato makubwa ambapo makato yake ni shilingi elfu tatu (3000) ikiwa ndio riba ya kulinda akaunti.


Aidha amewasisitiza wakulima kuacha mara moja biashara ya kahawa ya magendo kwani mtu akikamatwa anafanya hivyo serikali haitamuonea haya na atakuwa amejiingiza matatizoni bure kwani ni biashara haramu na isiyokubalika.
Ngara famers imefanya uchaguzi wake leo Agosti 31 ambapo imempata mwenyekiti na makamu wake na wajumbe wengine saba watakao iongoza kwa muda wa miaka mitatu.
Share:

Man United hali tete ligi kuu, yabanwa na Southampton ugenini


Klabu ya soka ya Manchester United imeendelea kujikuta ikiwa na wakati mgumu ndani ya ligi kuu nchini Uingereza msimu huu.

Timu hiyo Jumamosi hii imetoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Southampton ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo.

Man United ndio walikuwa wakwanza kupata goli dakika ya 10 kupitia kwa Daniel James, hata hivyo Jannik Vestergaard dakika ya 58.

Wakati huo huo mchezaji wa Southampton Kevin Danso alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 73 baada ya kuwa na kadi mbili za njano.

Kwa sasa United inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama tano na tayari imeshacheza michezo minne wakati Manchester City akiongoza akiwa na alama 10 akiwa amecheza michezo minne.

Share:

VIDEO: Kamanda wa zima moto na DC wafunguka katika tukio la moto


Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Gabriel Fabian Daqaro amesema kuwa moto unaondelea katika kiwanda cha Sunflag Kilichopo jijini Arusha umethibitiwa ambapo haujasambaa tofauni na kuteketeza Godaudi la Pamba huku Mkuu wa zima Moto Mkoa wa Arusha Semtana Yusuph akisema vifaa vipo vya kuthibiti moto yakiwemo magari

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USIKOSE KU SUBSCRIBE

Share:

VIDEO: IGP Siro adhibiti vitendo ya mauaji yatokanayo na imani za kishirikina


Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amemuagiza kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora kuhakikisha anashirikiana na wananchi katika kudhibiti vitendo vya mauaji yanayotokana na imani za ushirikina, ubakaji pamoja na uhalifu wa uvunjaji.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USIKOSE KU SUBSCRIBE

Share:

Serikali yawaonya wanaoshabikia Ndege ya ATCL kuzuiwa


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

Serikali imewatahadharisha watanzania ambao wanahusika au kushabikia kitendo cha ndege ya Shirika la ndege hapa nchini kushikiriwa na mahakama ya Afrika kusini, kwani kufanya hivyo ni sawa na kesi ya uhujumu uchumi.

Pia amebainisha kuwa ndege hiyo inashikiliwa kwa agizo la mahakama lakini Serikali ya Tanzania tayari imewasilisha hoja tatu nzito, juu ya tukio hilo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo (Agosti 31, 2019) Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali kwa mwezi Agosti 2019.

Dkt. Abas anasema kwa Sasa serikali hauwezi kusema chochote kwa sababu kesi ipo mahakamani, lakini tu ujumbe uwafikie wale wanaojihusisha na vitendo hivyo ni sawa na kesi ya uhujumu uchumi.

"Tunasubir majibu ya mahakama na tumewasilisha hoja nzito na watetezi upande wa pili wameanza kutetemeka, ujumbe kwa Hawa Sasa watanzania wenzetu wanaotuhujumu wajue tunasubir kesi iishe tutawashughulikia" amesema Dkt Abas.

Amesema kwa ujumla serikali haitakubali kuyumbishwa, na inaendelea na kuchapa kazi kuwatumikia watanzania, na haitarudi nyuma katika mapambano.

Aidha, Dkt Abbasi ameabainisha kuwa jumla ya shilingi bilioni 25.5 zimerejeshwa Serikalini kwa mchanganuo ufuatao; bilioni 14.6 ikiwa ni urejeshwaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu na bilioni 10.9 zilizotokana na thamani ya mali zilizotaifishwa yakiwemo magari, vituo vya mafuta, nyumba nane, magari nane na  Bilioni 20 ambazo ni mali zilizozuiwa kesi zikiendelea.

Amesema kuwa kwa upande wa Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imeokoa takribani shilingi bilioni 46.9 zilizokuwa zipotee kutokana na kutofuatwa taratibu za ununuzi, malipo ya zaidi ya mkataba kwa wakandarasi au baadhi kutorudisha fedha walizopewa kama dhamana na uzembe na rushwa.

Akizungumzia utekelezaji katika sekta ya uchukuzi, Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali imeanza zabuni ya kuagiza vichwa 22 (vitano vya mafuta yaani Diesel Locomotive na 17 vya umeme yaani Electrical Locomotive) na mabehewa ya abiria 60 na 1430 ya mizigo.

Aidha ameongeza kuwa, Serikali imeanza zabuni ya treni tano (5) zilizokamilika (Electrical Multiple Unit) za abiria zenye mabehewa nane (8) kila moja na vichwa viwili kwa ajili ya uendeshaji wa treni za abiria kwa kipande cha Dar es salaam hadi Morogoro na kisha Dodoma.

Mbali na hayo, ameeleza kuwa, Serikali imetenga fedha za ndani shilingi Bilioni 71.4 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja jipya la Mto Wami lenye urefu wa Mita 513.5 litakalojumuisha ujenzi wa barabara za KM 4.3 kwa kila upande ambapo kazi ya ujenzi huo imeshaanza.

Pia, Serikali imesaini mkataba wa shilingi bilioni 699.9 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja refu zaidi Afrika Mashariki na Kati la Kilometa 3.2 kuunganisha mikoa ya Mwanza na Geita kwenye eneo la Kigongo-Busisi katika Ziwa Victoria.

“Niwathibitishie Watanzania kuwa azma yetu ya kuiendeleza nchi kwa kasi chini ya Jemedari Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea kushika kasi na katika hili hakuna mwanadamu wa  kutuzuia wala kuturudisha nyuma” amesema Dkt Abbasi.
Share:

Mbunge Sugu aoa, Wabunge wa Chadema wamiminika


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) leo Jumamosi Agosti 31, 2019  amefunga ndoa takatifu na Mke wake, Happiness Msonga ambaye hivi karibuni walibahatika kupata mtoto mmoja.


Sugu na mkewe huyo wamefunga ndoa katika Kanisa Katoliki Ruanda Parokia ya Roho Mtakatifu lililopo jijini Mbeya.

Wabunge waliohudhuria ni pamoja na Anthony Komu , Lucia Mlowe, Sophia Mwakagenda na Lucy Mollel (wote Viti Maalum) Frank Mwakajoka (Tunduma), Joseph Haule (Prof. Jay), Joseph Selasini , David Silinde (Momba), Pascal Haonga (Mbozi) na Wilfred Lwakatare (Bukoba  Mjini).

Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Proffesor Jay ameandika "Hongereni sana kaka yangu @jongwe__ na Shemeji yetu Happiness msonga kwa kukamilisha ndoa yenu takatifu Leo, Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu Awabariki zaidi na awasiamie kwenye Maisha yenu ya NDOA, AMEN."
Share:

Humphrey Polepole awataka viongozi kujiongeza


Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amewaasa viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa kujiongeza kwa kuwa wabunifu ili kuacha alama ndani ya jamii.

Aidha amewataka wananchi kushirikiana katika masuala ya maendeleo ya jamii kwani maendeleo hayana chama.

Akizungumza katika hafla ya chakula cha hisani, kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa na madawati ,iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Kibaha,Polepole alisema baada ya kuteuliwa na mheshimiwa Rais ni lazima mhusika atengeneze uongozi uliotukuka kuwatumikia watanzania.

Anaeleza ,ugonjwa walionao baadhi ya viongozi wanashindwa kujiongeza kumpa heshima Rais dkt John Magufuli kutokana na uamuzi wa kuteuliwa.

Polepole amempongeza mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama ,kwa ubunifu wake ili kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu  na amemuahidi kumsemea mema.

“Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni ,mama nitakusemea ,hiki ulichokifanya ni kikubwa na viongozi wengine wanastahili kukiiga ,kwa maslahi ya watanzania ,ni lazima kiongozi aache alama katika jamii ,tengenezeni uongozi uliotukuka kwenye jamii zenu.”alifafanua Polepole.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amesema licha ya mkuu wa wilaya kufanya maamuzi hayo ,lakini serikali ni sikivu na imeshafanya mambo makubwa katika sekta ya elimu ikiwemo elimu bure ambapo imeshatoa milioni bilioni 20.5.

Pamoja na hilo, imeshatoa Bilioni 7.2 kwa ajili ya kukarabati shule nne kongwe ikiwemo Kibaha.
Ndikilo aliwaomba wadau waendele kujitokeza kusaidia kuchangia sekta ya elimu ili kupunguza changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo,miundombinu ya madarasa ,nyumba za walimu na madawati.

Awali mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter alieleza tatizo la upungufu  madarasa ilikuwa ni vyumba 65 ,lakini tangu kuanza kwa kampeni hii wameshapata fedha ambayo itaweza kujenga madarasa 40.

Amesema kwasasa imebakia madarasa 25 hivyo ameshukuru wadau kujitokeza kuwaunga mkono na ameomba ushirikiano huo uendelee.

Assumpter,ameomba jamii iondokane na dhana potovu kwamba ,ukianzisha ama kubuni suala la kuchangisha kwa ajili ya maendeleo kuna kuwa na rushwa ,au upigaji ,kwakuwa imani potovu kama hizo zinachelewesha maendeleo.
Share:

Waziri Lugola awataka Maafisa Uhamiaji kuepuka rushwa


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka Maafisa Uhamiaji nchini, kuepuka rushwa na kutokuwanyanyasa wageni na hasa wawekezaji nchini.


Akizungumza katika kikao cha Maafisa Uhamiaji Waandamizi kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Uhamiaji (Trita), Mjini Moshi, leo, Lugola alisema wawekezaji ni watu muhimu katika maendeleo ya nchi, hivyo wanaposumbuliwa kwa kunyanyaswa bila sababu za msingi ni kuvunja misingi ya uadalifu.


Pia Waziri Lugola aliwataka maafisa hao waache kutoa PI (tangazo la kuondolewa mtu asiye raia nchini) zenye utata kwa maslahi binafsi bila kuzingatia athari ambazo nchi inazipata.

“Yapo malalamiko kwamba kuna wageni wanaingia nchini na kuwekeza kwa ubia na Watanzania, biashara inapokuwa inaendelea Watanzania huwazunguka wageni na kuwatengeneza mazingira ya kuwafukuza ili wapate fursa ya kumiliki hizo biashara na hapo ndipo Idara ya Uhamiaji hutumika, acheni hayo mambo kwa kuwa yanatuchafua kama taifa letu,” alisema Lugola.

Aliongeza kuwa, Rais John Magufuli anatafuta wawekezaji kwa nguvu na kuwahakikishia usalama wao na biashara zao lakini baadhi ya watumishi wa umma badala ya kusaidia jitihada hizi wao wanatumika kuwafukuza kwa dhuluma.

Alisema wageni hao wakishafukuzwa na wanaacha uwekezaji wao nchini ambao wanadhulumiwa huko waliko wanaisema nchi vibaya na kwa uzoefu huo wageni wengine hawawezi kuja nchini.

“Tujitathimini, tuzingatie sheria, kanuni, taratibu na miongozo yetu kwa kuzingatia maslahi ya taifa, pia nawasihi sana mumsaidie mheshimiwa Rais kutimiza ahadi zake kwa Watanzania ambazo amezitoa kupitia Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na ahadi zake nyingine mbalimbali ambazo amekuwa akiahidi na kuzitekeleza,” alisema Lugola.

Aidha, Waziri Lugola kabla ya kukifungua kikao hicho kilichojumuisha Maafisa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, alisema kikao hicho kitakuwa chachu ya kudumisha maadili ya kazi, nidhamu, utii, na ushirikiano katika maeneo yao ya kazi ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya Idara hiyo ya Upendo, Mshikamano, Uwajibikaji na Kukataa Rushwa.

“Ni imani yangu kuwa, mtaendelea kutekeleza majukumu yenu kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma katika utoaji wa huduma bora kwa Wananchi,” alisema Lugola.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, alisema kikao hicho zitatolewa mada mbalimbali zitakazowasilishwa kuhusu rushwa na Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018 ambazo ndio mwongozo wa utendaji kazi wa  Idara ya Uhamiaji.

“Kwa kuwa Idara yetu ya Uhamiaji inatoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo pasipoti, vibali vya ukaazi, pasi pamoja na viza, hivyo kupitia kikao hiki tutazingatia kikamilifu mada hizo kwa kuwa zitatusaidia katika kutoa huduma bora kwa maslahi ya Idara yetu, Wizara na taifa kwa ujumla,” alisema Dkt. Makakala.

Share:

Dkt. Kigwangalla azindua kampeni ya 'Twenzetu Kutalii'


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizindua rasmi Kampeni ya “Twenzetu Kutalii” iliyoandaliwa na MISS Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune kuhamasisha Utalii wa ndani katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo, Dkt. Kigwangalla amewapongeza waandaaji wa tukio hilo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kutangaza Utalii ndani na nje ya nchi.

Amesema ipo haja ya viongozi na watu mashuhuri wakiwemo Wasanii kutumika kutangaza Utalii nchini. Amewataka wasanii wa Filamu waandae Filamu itakayoonesha na kubeba maudhui ya kuvitangaza Vivutio vya Utalii vilivyopo hapa nchini.

Aidha, ameiagiza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iendelee kutoa ushirikiano kwa Balozi huyo wa Utalii  MISS Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Makune kutokana na juhudi zake za kutangaza Utalii kwa vitendo.Pia ameiagiza TANAPA ianze kufanya mchakato wa kununua Meli mpya ya Kitalii itakayotumika Pwani ya Bahari ya Hindi.
Share:

Picha: Waziri Majaliwa azungumza na Waziri Mkuu wa Japan

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye hoteli ya The New Otani iliyopo Tokyo nchini Japan, Agosti 31, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezungumza na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe.


Share:

Heshima na hadhi ya Tanzania yaendelea kunga’ra Kimataifa


Heshima na hadhi ya Tanzania Kimataifa imeendelea kupanda kutokana na nia njema na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo (Agosti 31, 2019) Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali kwa mwezi Agosti 2019.

Dkt. Abaasi anasema: “kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa Julai 12, 2019 kwa pamoja kati ya Transparency International na Afro-Barometer, Tanzania imeongoza katika nchi 35 kwa kuonesha juhudi za wazi katika kupambana na rushwa”.

“Mafanikio haya yanatokana na msimamo thabiti wa Mhe. Rais Magufuli na Serikali yake katika kuimarisha taasisi muhimu kama vile TAKUKURU, Kuanzisha Mahakama ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi, mfumo wa udhibiti wa rushwa katika manunuzi kupitia PPRA”, ameongeza Dkt. Abbasi.

Akitolea mfano, amesema kuwa TAKUKURU imeokoa jumla ya shilingi bilioni 86 zilizotokana na mishahara hewa na ukwepaji kodi.

Aidha, Dkt Abbasi ameabainisha kuwa jumla ya shilingi bilioni 25.5 zimerejeshwa Serikalini kwa mchanganuo ufuatao; bilioni 14.6 ikiwa ni urejeshwaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu na bilioni 10.9 zilizotokana na thamani ya mali zilizotaifishwa yakiwemo magari, vituo vya mafuta, nyumba nane, magari nane na  Bilioni 20 ambazo ni mali zilizozuiwa kesi zikiendelea.

Amesema kuwa kwa upande wa Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imeokoa takribani shilingi bilioni 46.9 zilizokuwa zipotee kutokana na kutofuatwa taratibu za ununuzi, malipo ya zaidi ya mkataba kwa wakandarasi au baadhi kutorudisha fedha walizopewa kama dhamana na uzembe na rushwa.

Akizungumzia utekelezaji katika sekta ya uchukuzi, Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali imeanza zabuni ya kuagiza vichwa 22 (vitano vya mafuta yaani Diesel Locomotive na 17 vya umeme yaani Electrical Locomotive) na mabehewa ya abiria 60 na 1430 ya mizigo.

Aidha ameongeza kuwa, Serikali imeanza zabuni ya treni tano (5) zilizokamilika (Electrical Multiple Unit) za abiria zenye mabehewa nane (8) kila moja na vichwa viwili kwa ajili ya uendeshaji wa treni za abiria kwa kipande cha Dar es salaam hadi Morogoro na kisha Dodoma.

Mbali na hayo, ameeleza kuwa, Serikali imetenga fedha za ndani shilingi Bilioni 71.4 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja jipya la Mto Wami lenye urefu wa Mita 513.5 litakalojumuisha ujenzi wa barabara za KM 4.3 kwa kila upande ambapo kazi ya ujenzi huo imeshaanza.

Pia, Serikali imesaini mkataba wa shilingi bilioni 699.9 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja refu zaidi Afrika Mashariki na Kati la Kilometa 3.2 kuunganisha mikoa ya Mwanza na Geita kwenye eneo la Kigongo-Busisi katika Ziwa Victoria.

Katika Sekta ya Afya, Dkt Abbasi amesema kuwa, Serikali imeshatoa shilingi bilioni 30 kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa (RHH) na sehemu nyingi ujenzi umekamilika. Mikoa husika ni; Mwanza, Simiyu, Njombe, Songwe, Katavi, Geita na Dar es Salaam (Mwananyamala) na kuna Bilioni 3 imetolewa Kujenga Hospitali ya Kanda ya Wazazi Mbeya na shilingi bilioni 6.32 kujenga Hospitali ya Kanda Mtwara.

Vilevile, katika kuwekeza katika maisha ya watu ngazi ya Wilaya, Serikali mapema mwaka huu ilitoa shilingi Bilioni 105 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya 67 ambapo katika miaka zaidi ya 50 ya Uhuru tumekuwa na Hospitali katika Wilaya 77 tu; ndani ya mwaka huu mmoja zinajengwa 67 ambapo ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.

“Niwathibitishie Watanzania kuwa azma yetu ya kuiendeleza nchi kwa kasi chini ya Jemedari Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea kushika kasi na katika hili hakuna mwanadamu wa  kutuzuia wala kuturudisha nyuma” Amesisitiza Dkt Abbasi.
Share:

Waziri Biteko apiga marufuku shughuli za uchimbaji Madini ya Bauxite


Waziri wa Madini, Doto Biteko kulia akimsikiliza kwa umakini Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mazinde Juu wakati wa mkutano huo.


Waziri wa Madini Doto Biteko amepiga marufuku kuendelea kwa shughuli za uchimbaji wa madini ya Bauxite katika milima ya Bughai mpaka hapo utafiti wa athari za mazingira utakapofanyika.

Marufuku hiyo ameitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Magamba wilayani Lushoto wakati wa ziara ya kutembelea eneo hilo na baadae kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.

Amesema kuwa hakuna shughuli za uchimbaji zitakazofanyika mpaka hapo watakapoweza kupata majibu sahihi ya athari za kimazingira katika eneo hilo.
“Nimepiga mafuruku shughuli zote za uchimbaji kuendelea kwani nimeona kuna mashine kule za uchimbaji hivyo ziondoeni “amesema Waziri huyo.

“Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa wilaya naomba mlisimamie hili Lakini wakati tunaendelea kufanya hilo zoezi wale walikuwa na mashine pale lazima tujue ni wakina nani na wanapeleka wapi hiyo Bauxite “Alisema

Waziri huyo pia amemtaka Afisa Madini mkoa wa Tanga kufanya uchunguzi wa kiasi cha Madini kilichochimbwa ili kuweza kuwachukulia hatua wahusika wote waliochimba bila ya kufuata utaratibu kwa sababu hawajaruhusu uchimbaji kutoka wakati huo.

Awali akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliwataka wananchi kuwa wasikivu na kama kuna mahala wanahitaji ufafanuzi watapatiwa ili kuondoa sintofahamu kuhusiana uwepo wa madini hayo.

Alisema kwamba kumekuwa na haya madini watu wa madini watakuja kutoa elimu hapa na waziri amekuja kuja kuona haya madini na kuona namna ya kuyaendeleza.
Mkuu huyu wa mkoa alisema kama ipo sheria inasema nini na kama kuna suala la kisheria kwenye suala la uchimbaji lazima kuzingatiwe sheria na taratibu zilizopo kwa maslahi ya Taifa.

Awali akizungumza wakati wa ziara ya Waziri huyo Afisa madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho alimueleza Waziri huyo kwamba kwenye maeneo waliopewa ruhusu ya uchimbaji kuna mgogoro ulioanza muda mrefu tokea mwaka 2001 mpaka sasa.

Alisema kwamba hilo linatokana na wananchi kuwa na uelewa tofauti kuhusiana na uchimbaji wa Bauxite kwa ujumla kutokana na kuona kama utaondoa uoto wa asili na kuchafua mazingira kwa hiyo wananchi hawajaukubali mradi huo

Afisa Madini huyo Mkazi alisema pamoja na kwamba wadau wenye leseni za uchumbaji walichukua juhudi za kufanya utafiti za kuangalia athari za mazingira lakini lengo lao halikutimia kwa sababu wakati wakiendelea na mchakato huo ukaingiliwa.
Hata hivyo alisema inaonekana halmashauri na serikali wanaukubali huo mradi lakini wachache hawana uelewa kuhusu mradi huo kikubwa wananchi wanapaswa kupewa elimu kuhusiana na uchimbaji huo.
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger